YANGA HAITAFANYA DHARAU NA WACOMORO, LWANDAMINA ASISITIZA UMAKINI




Yanga imepangwa kuanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwavaa Ngaya de Mbe ya Comoros.

Kocha wake, George Lwandamina amesema haitakuwa kazi rahisi na Yanga haitafanya mzaha hata kidogo.

"Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni mikubwa na migumu, inakutanisha mabingwa wa nchi za Afrika. Hauwezi kuidharau timu yoyote," alisema.

Yanga ikifanikiwa kuwaondoa Wacomoro, itakutana na kati ya Zanaco ya Zambia au APR ya Rwanda ambazo ni timu ngumu.

Chini ya Lwandamina, Yanga imekuwa ikiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
YANGA HAITAFANYA DHARAU NA WACOMORO, LWANDAMINA ASISITIZA UMAKINI YANGA HAITAFANYA DHARAU NA WACOMORO, LWANDAMINA ASISITIZA UMAKINI Reviewed by Unknown on 2:03 PM Rating: 5

No comments:

Theme images by Colonel. Powered by Blogger.