EXCLUSIVE: HAJI MANARA APOTEZA UWEZO WA KUONA JICHO MOJA, MWENYEWE ASEMA HAJUI TATIZO NI NINI
Mkurugenzi
wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara, amepata
matatizo kwa kuwa amepoteza uwezo wa kuona baada ya jicho lake moja
kushindwa kuona.
Manara ambaye ni mcheshi anatumia jicho moja la upande wa kulia.
Akizungumza na SALEHJEMBE jijini Dar es Salaam, leo Manara amesema:
“Ni kweli nimepata tatizo, jicho la upande wa kushoto halioni na sijui sababu ni nini.
“Nimenichanganya
sana, tayari nimeanza matibabu. Nimechukua vipimo katika hospitali
kadhaa, hivyo siwezi kusema hali yangu ni nafuu, mbaya au nzuri hadi
nitakapopata majibu.
“Yeyote anayejua sehemu ambayo ninaweza kupata tiba bora kuhusiana na suala hili anaweza akanisaidia tafadhari,” alisema Manara.
SALEHJEMBE, INATOA POLE MANARA NA KUMTAKIA NAFUU MUNGU AMSAIDIE APONE HARAKA.
EXCLUSIVE: HAJI MANARA APOTEZA UWEZO WA KUONA JICHO MOJA, MWENYEWE ASEMA HAJUI TATIZO NI NINI
Reviewed by Unknown
on
2:10 PM
Rating:
No comments: