TFF YAWATAKA SIMBA KUHESHIMU KANUNI, PIA KUACHA KUDHARAU WAAMUZI WA TANZANIA
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limecharuka na kuitaka Simba kuonyesha heshima kwa kufuata utaratibu.
Kauli
hiyo ya TFF inafuatia ile kauli ya Simba ya kusisitiza inataka waamuzi
kutoka nje ya nchi na kama TFF isipofanya hivyo, watakapokutana na
watani wao wa jadi Yanga, hawatapeleka timu uwanjani.
Msemaji
wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema wao wataendelea kuwatumia waamuzi
wa Tanzania na kama Simba hawatapeleka timu, wao wanasubiri.
“Vizuri tukaheshimiana, watu wafuate taratibu na wajue waamuzi ndiyo wanaowachezesha mechi zao,” alisema.
“Sidhani
kama ni sahihi kuanza kupangua waamuzi wa nyumbani kwa kuwa tu watu
fulani hawataki. Kama wao hawatapeleka timu, sawa. Unawadharau
unapokutana na Yanga, lakini haohao wanachezesha mechi yako dhidi ya
timu nyingine kama JKT, Ndanda.”
Msemaji wa Simba, Haji Manara, juzi alisema wao hawatapeleka timu hadi TFF itakapotumia waamuzi kutoka nje ya Tanzania.
Manara alilalama kwamba waamuzi wamekuwa hawachezeshi kwa haki hasa Simba inapokutana na Yanga.
TFF YAWATAKA SIMBA KUHESHIMU KANUNI, PIA KUACHA KUDHARAU WAAMUZI WA TANZANIA
Reviewed by Unknown
on
9:53 AM
Rating:
No comments: