Stephano Mwasyika: Soka la Tanzania lina maadui wengi, malengo yangu ni kuwa kocha

img_1604
Na Baraka Mbolembole
“Nimecheza mechi nyingi nikiwa Tanzania Prisons, Yanga, Moro United na Taifa Stars lakini mechi ya Algeria 1-1 Tanzania mwaka 2012 siwezi kuisahau. Ilikuwa mechi ngumu sana, pia naikumbuka kutokana na fujo za mashabiki wao.” anasema mlinzi wa kushoto Stefano Mwasyika ambaye sasa amepona kabisa majeraha yake ya goti.
Mwasyika amevichezea vilabu vya Prisons 2007/08 na baada ya kufanya mambo makubwa ikiwemo kufunga magoli zaidi ya 8 katika ligi kuu msimu huo alisajiliwa na mabingwa wa kihistoria wa Tanzania timu ya Yanga SC ambako alicheza hapo hadi mwaka 2013.
Kwa sasa, Mwasyika ni mchezaji wa Friends Ranger inayocheza ligi daraja la kwanza pia yupo katika mafunzo ya ukocha kwa malengo ya baadae.
Mchezaji huyu amecheza VPL chini ya miaka kumi japokuwa ana uwezo na nguvu za kucheza aliamua kujiweka kando kwa sababu kadhaa zikiwemo chuki, na tabia za baadhi ya makocha wa VPL kutaka chochote kitu (10%) ili wamsaini.
“Maadui wa mpira wa Tanzania ni wengi sana. Mfano, mimi nimekuwa nikitangaziwa ni mkorofi, pia kuna baadhi ya makocha wana tabia ya kutaka kupewa asilimia fulani ya maslahi ya mchezaji ili wamsajili.”
“Mambo kama hayo pamoja na maumivu ya goti yalinifanya nikae pembeni na kujikita katika mafunzo ya ukocha kwa sababu umri unakwenda.”
“Napenda kuwa kocha wa mpira siku za usoni kwa sababu ni mchezo ninaoupenda na kuujua vizuri.” anasema Mwasyika mlinzi wa kushoto mwenye uwezo mkubwa wa kufunga magoli kutokana na mipira iliyokufa.
Hivi karibuni, Mwasyika alikuwa nchini Kenya, nilimuuliza kama anaweza kurejea VPL kama itatokea timu kumuhitaji wakati huu wa dirisha dogo la usajili.
Stephano Mwasyika: Soka la Tanzania lina maadui wengi, malengo yangu ni kuwa kocha Stephano Mwasyika: Soka la Tanzania lina maadui wengi, malengo yangu ni kuwa kocha Reviewed by Unknown on 6:23 AM Rating: 5

No comments:

Theme images by Colonel. Powered by Blogger.