MAHADHI AENDELEA MDOGOMDOGO TU HADI ENKA IKUBALI
Pamoja na kusumbuliwa na enka, kiungo mpya wa Yanga, Juma Mahadhi amesema ana matumaini atarejea.
Mahadhi
amekuwa akifanya mazoezi ya taratibu chini ya uangalizi wa daktari
wakati wenzake wakiendelea na mazoezi ya kawaida na magumu.
“Naendelea vizuri, nina matumaini nitapona kabisa,” alisema Mahadhi ambaye alionekana ni mtulivu.
Wachezaji wengine waliendelea na mazoezi kama kawaida chini ya Kocha Hans van der Pluijm.
Inaonekana
ubabe wa mabeki wa TP Mazembe hasa yule aliyemkanyanga ndiyo limekuwa
tatizo kwa Mahadhi ambaye amejiunga na Yanga akitokea Coastal Union.
Madhadhi
anaonekana kuwa hazina ya baadaye ya Tanzania kwa kuwa umri mdogo na
anaonyesha kuwa na kipaji hasa kama atajitunza na kutaka kujiendeleza.
MAHADHI AENDELEA MDOGOMDOGO TU HADI ENKA IKUBALI
Reviewed by Unknown
on
2:20 PM
Rating:
No comments: