KIBADA ONE YATINGA ROBO FAINALI NDONDO CUP 2016
Kibada One wamefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup baada ya kuichapa Madiba FC kwa magoli 3-1 kwenye uwanja wa Bandari, Tandika.
Magoli ya Kibada One yamekwamishwa kambani na Suleimani Mkonde, Yakubu Kibigi na Yahaya Zidi. Bao pekee la Madiba limefungwa na Stive Oswad.
Suleimani Mkonde alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo na haya ndiyo yalikuwa maneno yake: “Nawashukuru Clouds, Dr. Mwaka, Mwanaspoti na Startimes kwa kudhamini mashindano ili sisi tupate nafasi kama hizi za kuonekana.”
Kama kawaida ya michuano ya msimu huu, mchezaji bora akajinyakulia shilingi 50,000 kutoka gazeti la Mwanaspoti, timu iliyoshinda (Kibada One) imechukua shilingi 300,000 wakati timu iliyofungwa (Mdiba) wao wameambulia shilingi 200,000.
Dondoo muhimu
- Kibada ndiyo timu pekee ambayo ilipata pointi tisa kwenye hatua ya makundi ya michuano ya msimu huu.
- Kibada One imecheza michezo saba na kufanikiwa kushinda mechi sita na kutoka sare mchezo mmoja.
KIBADA ONE YATINGA ROBO FAINALI NDONDO CUP 2016
Reviewed by Unknown
on
2:27 PM
Rating:
No comments: