Majibu ya Wakala wa Samatta kuhusu kujiunga na AS Roma
Dirisha la usajili kwa nchi nyingi hasa za Ulaya limeendelea kushika kasi kwa vilabu mbalimbali kuendelea kuongeza wachezaji wapya ama kupunguza kwa maana ya kuuza na kununua.
Huku hapa Tanzania napo timu zikiendelea kujidhatiti kuliibuka taarifa ama fununu kuhusiana na mchezaji Mbwana Samatta anayechezea klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji kutakiwa kujiunga na klabu ya As Roma ya nchini Italia inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo yaani Serie A.
www.shaffihdauda.co.tz ikaona ni vyema kujua undani wa taarifa hizi na kukufikishia mpenzi wa soka na ilimtafuta moja kwa moja wakala wa Mbwana Samata Nicholas Onise kutoa ukweli wa mambo ambaye alikataa kwa haraka tu na kuashiria kuwa hakuna mazungumzo yaliyokuwepo ama yaliyokuwa yamefanyika kumuhisha Samata kuelekea nchini Italia kama ilivyokuwa imeripotiwa awali. Onise amekanusha na kudai kuwa Samatta ni mchezaji wa Genk ana atacheza Genk.
Majibu ya Wakala wa Samatta kuhusu kujiunga na AS Roma
Reviewed by Unknown
on
2:46 PM
Rating:
No comments: