KIPA LA MEDEAMA LATUA RASMI SIMBA
Wekundu
wa Msimbazi Simba SC wamethibitisha kumsajili kipa mpya Mghana Daniel
Agyei aliyekuwa akikipiha kunako klabu ya Medeama ya nchini humo.
Kipa huyo ameondoka kwenye klabu hiyo maarufu kwa jina la Mauves baada ya kucheza kwa kipindi kisichozidi msimu mmoja.
Kupitia akaunti ya Instagram Simba wamethibitisha hilo kwa kuweka picha yake yenye maelezo yanayosomeka: "Golikipa Daniel Agyei amewasili rasmi nchini tayari kujiunga na kikosi cha Simba.
Agyei
,24, alijiunga na Medeama SC katika raundi ya pili ya msimu kwenye
Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Ghana Premier League baada ya kurejea
kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akicheza kunako klabu ya Free
State Stars.
Mapema mwezi huu Agyei aliandika kwenye moja ya akaunti zake za mitandao ya kijamii kuthibitisha kuondoka kwake klabuni hapo.
“Sidhani
kama kuna maneno yatakayotosheleza kiasi cha huzuni ninayoisikia
kutokana na kuwaaga wote hapa kwenye klabu yangu pendwa ya Medeama SC, "
alindika kwenye akaunti yake ya Facebook.
“Ningependa
kuwashukuru viongozi, benchi la ufundi, wachezaji wenzangu pamoja na
mashabiki kwa sapoti yao kubwa waliyonionesha kwa kipindi kifupi
nilichodumu klabuni hapa. Medeama itabaki kuwa klabu itakayodumu moyoni
mwangu milele.”
KIPA LA MEDEAMA LATUA RASMI SIMBA
Reviewed by Unknown
on
5:56 AM
Rating:
No comments: