NGASSA ADONDOKEA MBEYA CITY
Sasa
imedhihirika!! Baada ya tetesi ya takribani siku mbili mfululizo,
kiungo mshambuliaji wa pembeni Mrisho Ngassa sasa ni rasmi mali ya Mbeya
City.
Ngassa
ameonekana kwenye picha pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano wa Mbeya City FC Dismas Ten wakiwa wameshika mikono ikiwa ni
ishara ya kumkaribisha nyota huyo wa zamani wa Yanga klabuni hapo.
Safari ya Ngassa kutua Mbeya City imekuja baada ya kuachana na klabu ya Free State Stars FC ya Afrika Kusini na Fanja ya Oman.
Bado haijawekwa wazi ni mkataba wa muda gani ambao Ngassa amesaini na Wagonga Nyundo hao wa jiji la Mbeya.
NGASSA ADONDOKEA MBEYA CITY
Reviewed by Unknown
on
6:00 AM
Rating:
No comments: