MCHEZAJI WA TIMU YA MWANANYAMALA AANGUKA NA KUZIMIA UWANJANI, AKIMBIZWA HOSPITALI
SIKU ISMAIL ALIPOANGUKA UWANJANI NA KUPOTEZA MAISHA |
Siku
chache baada ya kinda wa Mbao FC timu ya vijana U 20 kuanguka uwanjani
na kupoteza maisha, mchezaji mwingine ameanguka na kuzimia.
Katika
hali isiyotarajiwa, beki wa timu ya Colombia FC ya Mwananyamala,
Athumani Suwa, jana asubuhi alikata kauli baada ya kuzimia uwanjani
kutokana na kugongana na mwenzake wakati wakiwania mpira kabla ya
kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar.
Tukio hilo lilitokea katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala B, Dar.
Baada
ya kufika hospitalini hapo na kushuhudia mchezaji huyo akiwa amewekwa
katika chumba cha mapumziko baada ya kupatiwa huduma.
Akizungumza
mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ambaye alikuwepo katika mazoezi hayo,
Ramadhan Ally, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo uwanjani.
MCHEZAJI WA TIMU YA MWANANYAMALA AANGUKA NA KUZIMIA UWANJANI, AKIMBIZWA HOSPITALI
Reviewed by Unknown
on
5:45 AM
Rating:
No comments: