SIMBA KUHAMIA MOROGORO JUMAPILI, OMOG ATAANZA YAKE HUKO
Kikosi cha Simba, kimeanza maandalizi ya msimu mpya chini ya Kocha mpya, Joseph Omog.
Omog
raia wa Cameroon ameanza kuinoa Simba katika Uwanja wa Chuo cha Polisi
eneo la Kilwa Road jijini Dar es Salaam ambako mashabiki hawaruhusiwi
kuingia kama alivyotaka.
Jumapili, Simba itahama jijini Dar es Salaam kwenda Morogoro kwa ajili ya kambi maalum.
“Kweli
kocha amesema hapa ni kama kupasha misuli na baada ya hapo tutaanza
kambi rasmi Morogoro. Kule tunakwenda Jumapili,” kilieleza chanzo kutoka
ndani ya Simba.
SIMBA KUHAMIA MOROGORO JUMAPILI, OMOG ATAANZA YAKE HUKO
Reviewed by Unknown
on
6:06 AM
Rating:
No comments: