Michezo Walipofikia Juventus na Man United kuhusu Paul Pogba

 

Baada ya kocha wa Manchester United Jose Mourinho kutambulishwa Old Trafford alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa mipango yao kwa sasa ni kusajili wachezaji wanne na kati ya hao watatu tayari wameshafanikiwa kuwasajili ila anaamini mmoja atafanikiwa kumsajili mapema pia bila kumtaja jina.
July 7 2016 taarifa kutoka Italia zilizoripotiwa na Di Marzio ni kuwa kocha Jose Mourinho anajiandaa kumsajili staa wake wa nne ambaye ni Paul Pogba na tayari wameshafikia katika makubalina na klabu ya Juventus anayoichezea staa huyo.
Man United wamekubaliana na Juventus dau la uhamisho wa Pogba, ambaye atakuwa analipwa mshahara wa Pound milioni 11.1 kwa mwaka, Pogba kama akisajiliwa na Man United atakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Man United chini ya Jose Mourinho, baada ya kusajiliwa kwa Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.
Michezo Walipofikia Juventus na Man United kuhusu Paul Pogba Michezo Walipofikia Juventus na Man United kuhusu Paul Pogba Reviewed by Unknown on 6:16 AM Rating: 5

No comments:

Theme images by Colonel. Powered by Blogger.