PLUIJM AELEZEA SABABU YA MAZOEZI YA YANGA KUWA "KAZI KAZI" TU
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameeleza sababu ya mazoezi ya Yanga kuwa ya nguvu kazi utafikiri mechi.
Pluijm raia wa Uholanzi, amesema lazima mazoezi yawe magumu ili kuhakikisha yanaenda na uhalisia.
“Tunahitaji
kucheza kwa kasi, kwa nguvu. Tunashambulia na kulinda pamoja. Haya yote
lazima yafanyike mazoezini. Uhalisia ndiyo unatengeneza ubora sahihi,”
alisema Pluijm.
Katika mazoezi ya Yanga, wachezaji wamekuwa wakicheza ngangari kweli utafikiri ni mechi hasa.
Baadhi
wamekuwa wakipata hofu huenda wanaweza kupata majeraha lakini mazoezi
hayo yamekuwa yakisifiwa na mashabiki kwamba ni mazoezi hasa na hakuna
utani.
PLUIJM AELEZEA SABABU YA MAZOEZI YA YANGA KUWA "KAZI KAZI" TU
Reviewed by Unknown
on
5:58 AM
Rating:
No comments: