TP MAZEMBE WAJIFUA TAIFA KWA UFICHO, WAZUIA MASHABIKI, WAANDISHI KUWAONA
Kikosi cha TP Mazembe wamejifua kwa nusu saa tu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
TP
Mazembe kutoka DR Congo wako nchini kuwavaa Yanga katika mechi ya Kombe
la Shirikisho, mechi itakayipigwa kesho kwenye uwanja huo.
Wachezaji wao walipoingia uwanjani hapo, walinzi walioongozana na kikosi hicho walianza kuzuia watu kuingia uwanjani hapo.
Walizuiwa
watu mbalimbali wakiwemo waandishi na inaonekana Mazembe walijifua
haraka na kwa muda mfupi na baada ya hapo walipanda basi na kurejea
hotelini.
TP MAZEMBE WAJIFUA TAIFA KWA UFICHO, WAZUIA MASHABIKI, WAANDISHI KUWAONA
Reviewed by Unknown
on
4:39 PM
Rating:
No comments: