MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE KURUSHWA LIVE NA SUPER SPORT
Wakati
malumbano ya nani ataonyesha mchezo kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe,
sasa taarifa rasmi zimetolewa kuwa DStv wataurusha mchezo huo.
DStv kupitia Super Sport wataurusha mchezo huo moja kwa moja.
Meneja Mkuu wa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu amethibitisha kuhusiana na hilo, leo.
"Kweli Super Sport wataurusha mchezo huo moja kwa moja. Hivyo itakuwa nafasi nzuri kwa mashabiki nchini kufaidika.
"Ni
mechi kubwa kwa Tanzania na Afrika kote, hivyo mashabiki waitumie nafasi
hiyo kwa kuhakikisha wanalipia ving'amuzi vyao ili wasipitwe," alisema.
Yanga inaivaa TP Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho ambayo mashabiki wataingia bila kulipa kiingilio.
Tayari
mechi hiyo ni gumzo kwa kuwa mashabiki wa Yanga wataingia bila
kiingilio na wametakiwa na uongozi wa Yanga kujitokeza kwa wingi.
MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE KURUSHWA LIVE NA SUPER SPORT
Reviewed by Unknown
on
4:33 PM
Rating:
No comments: