JICHO LA 3: YANGA VS TP MAZEMBE NATAKA KUMUONA ‘KAMUSOKO’ NA FABREGAS WA RWANDA
Na Baraka Mbolembole
YANGA SC tayari wamefanya mambo mengi muhimu nje ya uwanja kuhakikisha wanapata ushindi katika game yao ya pili na ya kwanza katika uwanja wa nyumbani watakapoikabili TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi katika michuano ya CAF Confederation Cup.
Mchezo huo utapigwa ndani ya dimba la uwanja wa Taifa, Dar es Salaam siku ya Jumanne hii. KIKOSI CHA USHINDI Kocha, Hans Van der Pluijm hajawahi kuniangusha katika upangaji wa kikosi chake na game plan zake mara zote zimekuwa zikibadilikabadilika kutoka na aina ya timu na umuhimu wa mchezo.
Na mara zote vikosi vyake vimekuwa na dhamira ya kusaka ushindi, kufungwa au sare ni matokeo ya ziada na yanakubalika katika mchezo wa kiungwana kama ‘mpira wa miguu.’
Kumpanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ kama kipa chaguo la kwanza ni mtazamo wa kila mtu na kipa huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania anaweza kuingia katika orodha ya makipa bora mwisho wa michuano kama ataendeleza kiwango chake kile ambacho alikionyesha katika game dhidi ya Al Ahly 2-1 Yanga (Cairo,) Yanga 2-0 Esperanca (Taifa), Esperanca 1-0 Yanga (Angola) na MO Bejaia 1-0 Yanga (Algeria.)
Dida amekuwa imara katika uchezaji wa krosi, lakini kikubwa katika game ya kesho anapaswa kuongeza umakini, ujuzi na uwezo wa kuruka kwa kuwa Mazembe itafanya mashambulizi mengi, lakini watategemea zaidi mikwaju ya mbali yenye uelekeo sahihi golini kwa Yanga kwa maana wachezaji wao wengi wa nafasi ya kiungo ni wachezesha timu wenye ubunifu wa kupiga pasi za hatari na kiki za mbali.
Hans kama nilivyo mimi angependa sana kufanya mabadiliko baadhi kutoka katika kikosi kilichopoteza game ya kwanza ugenini dhidi ya MO Bejaia na bila shaka, Hassan Kessy Ramadhani angechukua nafasi ya Mbuyu Twite katika beki namba mbili. Yanga wanahitaji ushindi katika mchezo wa kesho ili kuleta usawa katika kundi la kwanza.
Kumpanga Kessy badala ya Mbuyu kuna faida kubwa katika mashambulizi. Mbuyu hukaba vizuri na upande wa wing namba 11 wa Mazembe umekuwa ni mwongozo wa matokeo mazuri ya timu hiyo. Mazembe wanapenda kupeleka mbele mashambulizi yao kupitia sehemu za pembeni za uwanja. Kama ni tahadhari, Mbuyu na Oscar Joshua ni machaguo ambayo Hans anaweza kuyapanga na kuifanya timu yake kucheza katika umakini katika beki.
Kama fullbacks zitayumba itaiangamiza safu yote ya ulinzi kwa hivyo basi, kama Mbuyu atapangwa kama mlinzi wa kulia, angalau atapaswa kutengeneza walau nafasi 3 za kufunga na kubaki nyuma tu kama ilivyokuwa katika game ya wiki iliyopita. Yanga inategemea mipira ya pembeni ambayo hupigwa na walinzi wa pembeni.
Kessy ni injini ya kupandisha mashambulizi, ana kasi na krosi zake pasi huwa zenye mwelekeo. Kama atacheza hakitaharibika kitu na anaweza kufanya vizuri zaidi ya tulivyozoea kuona Yanga ikicheza ikiwa na Mbuyu au Juma Abdul katika beki namba mbili.
Kama ningekuwa katika nafasi ya Hans ningewapanga, Kelvin Yondan, nahodha, Nadir Haroub na Mtogo, Vicent Bossou katika beki ya kati na ningeicheza timu yangu katika mfumo wa 5-3-2. Huu ni mfumo mzuri kwa timu ndogo pindi inapocheza na timu kubwa.
Yanga ni wadogo kwa Mazembe lakini kwa aina ya walinzi wao wa pembeni (Mbuyu, Kessy, Oscar, J.Abdul) watashambulia sana lango la Mazembe na hawatapoteza umakini katika beki ya kati ambayo itapaswa kucheza katika hadhi ya kiwango cha kimataifa.
Yanga hawatapaswa kucheza za wazi lakini ili wapate matokeo watapaswa pia kucheza faulo za kitaalamu dhidi ya Mzambia, Rainford Kalaba na Mghana, Solomon Asante. Ni lazima mabeki na hata wachezaji wa nafasi ya kiungo wajiandae kucheza tackling sahihi.
Mazembe wanapasiana sana, pia wana kasi, wajuzi, na wanajua kupanga mashambulizi yaliyokamilika. Bila ‘faulo za kitaalamu’ si rahisi kuwashinda ila Yanga watawashinda tu.
NATAKA KUMUONA ‘MAN-KAMUSOKO’ SASA, NA FABRIGAS WA RWANDA
Yanga haitakuwa na sababu tena za kujitetea ikiwa watapoteza mchezo wao wa pili katika kundi. Ikiwa na Thaban Kamusoko mmoja wa viungo bora zaidi katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu uliomaomalizika, Haruna Niyonzima ‘Fabregas,’ huku Saimon Msuva, Deus Kaseke, Geofrey Mwashuiya, na ingizo jipya katika timu, Juma Mahadhi dhidi y a Mazembe wanataka kuwaona wakitimiza matarajio yetu, kuona Mazembe kwa namna yoyote ikiacha pointi 3.
Yanga haikuwahi kupata ushindi wowote katika game 7 za hatua ya makundi katika michuano ya CAF. Baada ya kupoteza dhidi ya Raja, Manning Rangers, Asec (Caf Champions league 1998,) kisha dhidi ya MO Bejaia katika Confederation Cup msimu huu, mechi ya 8 kwanza ni dhidi ya mabingwa mara tano wa ligi ya mabingwa na wanakuja wakiwa na viungo wawili mahiri sana wanaocheza ndani ya Afrika ( Asante na Kalaba.)
Nina hamu na shahuku ya kumuona Kamusoko akiwazima wacheza timu hawa kwa kushirikiana na Bossou kama viungo wa ulinzi. Nataka kumuona Kamusoko akikaba na kupiga pasi za kwenda mbele huku akizifuata, nasubiri kuona kama Mzimbabwe huyu atapiga pasi zake za kupenyeza, naimani nitaendelea kuona utululivu wake na pasi za haraka za kupandisha mashambulizi ya kustukiza. Hii ni mechi ya Mzimcabwe huyu?
Nasubiri, hadi sasa ndiye dimba la kati makini na bora zaidi katika ligi ya Bara, ila bado namsubiri kumpa vyeo vingine. Kuwapanga Kamusoko, Niyonzima na Juma Mahadhi katika kiungo, kisha Obrey Chirwa na Donald Ngoma katika safu ya mashambulizi itakuwa ni kikosi kabambe, pia wanaweza kuingia Msuva au Kaseke katika kikosi cha kwanza lakini halitakuwa jambo zuri kwa Yanga kwa maana wanakutana na timu isiyojilinda hata ikicheza ugenini.
Baada ya game tutaongea zaidi ila imani yangu Yanga itaichapa Mazembe na haitapoteza mchezo wa kimataifa Dar es Salaam.
JICHO LA 3: YANGA VS TP MAZEMBE NATAKA KUMUONA ‘KAMUSOKO’ NA FABREGAS WA RWANDA
Reviewed by Unknown
on
4:57 PM
Rating:
No comments: