NGASA, SHAMTE, HATIHATI MBEYA CITY VS TOTO
NGASA, SHAMTE, HATIHATI MBEYA CITY VS TOTO
WAKATI
‘raundi ya 17 ya ligi kuu Tanzania bara ikitaraji kuendelea Ijumaa na
Jumamosi hii, kikosi cha Mbeya City FC kimeendelea na mazoezi ikiwa ni
matayarisho ya mchezo namba 130 dhidi ya wageni Toto Africans ya
Mwanza uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kwenye
mazoezi ya timu hiyo jana asubuhi, Ofisa habari wa kikosi hicho Dismas
Ten amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na
wachezaji wote wakiwa na ari kubwa licha ya kuwepo kwa taarifa za
majeraha kwa mlinzi Haruna Shamte aliyeumia kwenye mchezo uliopita dhidi
ya Kagera Sugar.
“Kama
unavyofahamu Jumamosi iliyopita tulipata suluhu ya 0-0 na Kagera Sugar,
mara hii tunafanya maandalizi makubwa kuhakiksha tunashinda mchezo
ujao, pointi tatu ni jambo pekee linalohitajika kwenye duru hii ya pili,
tunaifahamu Toto kuwa ni timu nzuri lakini mara kadhaa sisi tumekuwa
tunaibuka wababe dhidi yao,” alisema.
Akiendelea
zaidi Ten aliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo dhidi ya Toto, City
inaweza kukosa huduma ya mlinzi wake Haruna Shamte aliyepata majeraha ya
kifundo cha mguu kwenye mchezo uliopita ingawa jopo la madaktari
wameahidi kutoa taarifa mpya juu yake siku ya kesho (leo) huku
akigusia pia suala la ITC ya kiungo Mrisho Ngassa.
“Shamte
alipata majeraha kwenye mchezo uliopita, huenda asiwepo kikosini
Jumamosi, ingawa hili litategemea na ripoti ya daktari siku ya kesho
(leo), kuhusu Mrisho Ngassa ni kweli ITC yake ilichelewa, hii ni kwa
sababu Ijumaa na Jumamosi ni siku ya mapumziko huko Oman, tulizungumza
nao jana (juzi) wakaahidi kututumia leo (jana), hivyo tuna uhakika leo
(jana) wataituma na ni wazi atakuwa sehemu ya kikosi kwenye mchezo
huo,” alimaliza.
Imetolewa na Mbeya City FC
NGASA, SHAMTE, HATIHATI MBEYA CITY VS TOTO
Reviewed by Unknown
on
2:20 PM
Rating:
No comments: