KIPA MHISPANIA ASEMA YUKO TAYARI KWA USHINDANI AZAM FC NA LIGI KUU BARA
Kipa
wa zamani wa Tenerife ya Hispania, Juan Jesus Gonzalez amesema yuko
tayari kwa ushindani licha ya kwamba ni mara yake ya kwanza kucheza
barani Afrika.
Jesus yuko nchini kwa ajili ya kufanya majaribio ili ajiunge na Azam FC kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza leo na SALEHJEMBE, Jesus amesema matarajio ya ushindani mkubwa ni jambo jema kwake.
"Nataka kushindana na kufanya vizuri, najua Azam ni timu kubwa Tanzania. Nitaonyesha uwezo wangu," alisema akionyesha kujiamini.
Kipa
huyo mtaratibu, ametua nchini tayari kwa ajili ya kujiunga na Azam FC
kama watakubaliana na uongozi wa klabu hiyo ambayo ndiyo mpinzani mkubwa
wa watani Yanga na Simba.
KIPA MHISPANIA ASEMA YUKO TAYARI KWA USHINDANI AZAM FC NA LIGI KUU BARA
Reviewed by Unknown
on
3:03 PM
Rating:
No comments: