Matatu aliyotangaza Manji baada ya kuchukua fomu kugombea tena Yanga
Siku moja baada ya katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit na afisa habari wa Yanga Jerry Muro kutangaza kuwa uchaguzi wao utasimamiwa na wao wenyewe na sio shirikisho la soka Tanzania TFF kama ilivyokuwa imetangazwa na baraza la michezo, mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji leo aliongea na waandishi wa habari.
Yusuph Manji akiwa na makamu mwenyekiti wake Clement Sanga
Manji amechukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo kwa awamu nyingine tena na kutangaza mambo matatu, moja kutoa sauti inayothibitisha kuwa TFF na baadhi ya watu wanahujumu uchaguzi wa Yanga, mbili kasimamisha uanachama wa wanachana waliosikika kwenye audio clip inayosadikiwa kuwa ya kupanga hujuma na wale waliochukua fomu TFF.
Baada ya Manji kufanya hivyo alimaliza kwa kumuagiza mkuu wa idara ya habari wa Yanga Jerry Muro kuandika barua kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU na kuomba ufanyike uchunguzi kuhusu hujuma za uchaguzi wa Yanga ambao TFF wanadai kuwa wataratibu wao lakini Yanga hawakubaliani na hilo.
Matatu aliyotangaza Manji baada ya kuchukua fomu kugombea tena Yanga
Reviewed by Unknown
on
4:23 AM
Rating:

No comments: