GRIEZMANN AIBEBA UFARANSA MGONGONI HADI ROBO FAINALI EURO 2016 By Dick Dauda - June 26, 2016


Timu ya taifa ya Ufaransa ambao ndiyo wenyeji wa michuano ya Euro 2016 wametoka nyuma na kuifunga Jamhuri ya Ireland kisha kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Kikosi cha Ireland kilitangulia kupata bao na kuongoza kuanzia dakika ya pili baada ya Robbie Brady kupachika bao kwa mkwaju wa penati kufuatia Shane Long kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.
Lakini Ufaransa walikuja juu na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Antoine Griezmann ambaye alifunga kwa kichwa kabla ya kuzamisha bao la pili na la ushindi la ushindi kwa wenyeji wa michuano hiyo.
Shane Duffy alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea vibaya Griezmann na kuiacha timu yake ikicheza pungufu.
Kikosi cha Didier Deschamps kitapambana na England au Iceland kwenye hatua ijayo mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Stade de France Jumapili July 3.
GRIEZMANN AIBEBA UFARANSA MGONGONI HADI ROBO FAINALI EURO 2016 By Dick Dauda - June 26, 2016 GRIEZMANN AIBEBA UFARANSA MGONGONI HADI ROBO FAINALI EURO 2016 By Dick Dauda -  June 26, 2016 Reviewed by Unknown on 8:58 AM Rating: 5

No comments:

Theme images by Colonel. Powered by Blogger.